SERGE MUKOKO TONOMBE, EXPRESS YOURSELF

SERGE MUKOKO TONOMBE, EXPRESS YOURSELF

Alichukuliwa Pele kutoka mitaa ya Sao Paulo alipokuwa anacheza na tabasamu usoni na kufunga kwa kuburudisha sana, lakini alipopelekwa kwenye soka la kitabuni akafeli kuonesha alichonacho na tabasamu likapotea usoni

Watu wengi waligundua Pele hafurahii tena mpira wake, Kocha akamwita na kumwambia ebu cheza kama unavyocheza kule mitaani kwenu Sao Paulo, ndipo hapo Pele akaibadili historia ya dunia kwenye soka, alicheza kwa tabasamu na kuonesha kipaji chake

Dunia ya Pele ikapita zake, ikaja dunia nyingine tena ya Ronaldinho Gaucho, alianza kuonesha meno na tabasamu lake 1999 Brazil vs Venezuela kwenye Copa America, anachukua mali anawatoka mabeki huku anacheka, anamchukua Kipa na kuwasubiri tena mabeki kisha anafunga

Dunia ikashindwa kuelewa ni aina gani hii ya binadamu ambaye akapigwa kiatu bado anacheka, akipewa kadi anacheka, alipoambiwa Real Madrid hawatomsajili kisa hana mvuto alicheka, lakini alifanya kitu kibaya Bernabeu miaka michache baadae na Mashabiki walimpigia makofi, anatoka Uwanjani huku anacheka

Ikapita dunia ya Gaucho, dunia ya vipaji halisi na tabasamu zito usoni, ikaja dunia moja kutoka Kongo ya Kinshasa anaitwa Serge Mukoko Tonombe, kipaji kingine kikubwa kinachocheza uvunguni ambacho kina furaha na amani muda wote

Aina yake ya mpira vitabu vya soka wanaita EXPRESS YOURSELF PHILOSOPHY, cheza mpira kwa kufurahi usiwe na hofu, cheza mpira kwa kuburudisha usiwe na papara, hichi ndicho anafanya Mukoko, nyuma ya tabasamu lake amejinakshi na kanuni ya FIFA, My Game is Fair Play

Kwanza nimpe shukrani mpiga picha kwa hii picha adhimu, misuli imewaka moto na damu zimechemka haswa, chini yupo Edward Charles Manyama wa Namungo amelala analia, hakuna wa kumpa pole, lakini Mukoko na tabasamu lake anashuka kumpa pole

Ni binadamu wachache kwenye eneo lake wenye moyo kama wake, tangu zama za Roy Keane, Makelele na wengine ila yeye kaja kuiweka picha ya Ronaldinho kwenye eneo la Patrick Viera

Mukoko Tonombe EXPRESS YOURSELF 🙏🤝


#salushinetz 

Post a Comment

0 Comments