SIMBA SC, WELCOME INTO THE BADLANDS

SIMBA SC, WELCOME INTO THE BADLANDS

Kwanza niwape heshma wale wote waliotengeneza historia ya Simba kwenye michuano ya Afrika, naikumbuka vyema historia tukufu ya 1976, awape pumzi wote mlio hai na awape pumziko la milele mliotangulia, mbele yenu nyuma yetu

Pili nimpe pongezi Captain Fantastic Madaraka Suleiman 'Mzee wa Kiminyio'  na jeshi lake la 1993 wanacheza fainali ya Kombe la Washindi dhidi ya Stella Abdijan, nakumbuka kuna simulizi nyingi sana juu ya fainali ile lakini Simba inahitaji sana Captain kama Madaraka

Usiku kuelekea fainali mkondo wa pili, inasemekana Mzee wa Kiminyio alitonywa na Mashabiki kuwa Marsha, Mwameja na George Masatu wapo Bilcanas wanakula bata, basi Captain alijibeba mpaka pale na kuleta ubabe wake kisha kuwatoa jamaa klabuni

Hii yote ni harakati za kuifanya Simba ifanye makubwa sana barani Afrika, kwenye hiyo Ardhi ya vita (Badlands) hakuna kitu rahisi, hakuna mchezo rahisi bali kila kitu ni Jihad kubwa ili kupata matokeo, ni jasho, visasi na damu humwagika

Karibuni tena kwenye uwanja wa vita, wenye rafu nyingi na matukio mengi ya kutisha ila Simba ikamvua ubingwa Zamalek ya Misri 2003 na kuitangazia Afrika kuwa kiti kipo huru na bingwa mpya apatikane, historia imeandikwa na itamsoma kama Suleiman Abdallah Matola Veron kama Nahodha wa Kikosi kile

Historia itaendelea kusomwa juu ya Smart defender Victor Costa Nyumba, anamaliza dakika 90 bila jezi kuchafuka lakini ni Centre half huyo, historia itasomwa juu ya Christopher Alex Massawe moja kati ya Wachaga wachache kwenye historia ya soka, lakini mikono salama ya Juma K Juma

Hii sio mara ya kwanza Simba kuingia kwenye ardhi ya vita (badlands) aliingia pia 2018 kwa miguu salama ya Clatous Chota Chama, kisha Chama huyo huyo kuwapeleka nusu fainali, Ngamia alipita kwenye tundu la sindano, Mamba alitukanwa kisha wakavuka mto Bwana, sio wageni kwenye vita

Karibuni tena Badlands, safari ya Cairo sio ngeni kwenu tunasubiri vita yenu na Mzulu Pitso Mosimane, safari ya Sudan sio ngumu kwenu tunaikumbuka miguu ya Patrick Mutesa Mafisango na safari ya AS Vita sio ngeni kwenu, mnaifahamu ramani basi mtafahamu wapi pa kupita

WELCOME AGAIN INTO THE BADLANDS, SIMBA🇹🇿

#salushinetz

Post a Comment

0 Comments