CRISTIANO RONALDO NA NDOTO YAKE KWA CRISTIANO JR


 

 

 CRISTIANO RONALDO NA NDOTO YAKE KWA CRISTIANO JR

"Kaka kwenye umri kama wa Mwanangu mimi nilikuwa na njaa kali ya mafanikio, sikuwa na uhakika wa kula hivyo kila siku uwanjani ilikuwa vita ya mafanikio kwangu"

Yalikuwa ni maneno ya Cristiano Ronaldo akiongea na rafiki yake Khabib bingwa wa UFC, Ronaldo akiamini kuwa huenda Mwanae asiwe na njaa kama yake kwakuwa tayari ana kila kitu

Ronaldo kuna muda alilazimika kusafiri na Familia yake Mpaka Ureno, kisiwani kwao Funchal Madeira kwenye mtaa wake wa asili wa San Antonio, yote hii ni kumpa hasira Mwanae, ajue maana ya Maisha

Mtoto wake alipewa Rafiki yake Miguel Paixao waliokuwa Wana tangu zamani kisha Mkewe Georgina alikuwa na Kaka wa Ronaldo anaitwa Hugo, walizungushwa kila Mtaa na kila hatua Ronaldo alipitia mpaka alipo leo, machozi nusu yawatoke

Eneo la San Antonio ni Kaskazini Mashariki mwa kisiwa cha Madeira, kuna majengo marefu ya zamani, hapo kuna mchanganyiko wa Wazungu na watu weusi ndio Ronaldo alikuwa anaupiga mpira eneo hatarishi sana, Mwanae aliumia sana kuona palivyo

Ronaldo anamjenga kisaikolojia Mwanae na Mkewe ili Mtoto apambane na Mkewe apambane kuwasimamia watoto, ndio maana amekuwa akihudhuria mechi karibia zote za Watoto Juventus

Cristiano Jr akirejea nyumbani hali vyakula laini, bali ni diet maalum inayosimamiwa na Daktari wa Baba yake, inaaminika wameanza kumjenga kifiziki kuenda na mikiki ya soka, ndio maana kwenye umri wake yupo fit sana

Cristiano Jr akitoka mazoezini au kwenye mechi anaingizwa kwenye barafu, maumivu yake yanatibiwa kwa barafu na kuanza kumjenga misuli ingali mdogo, kitaalamu wanalimit Inflammatory reaction

Baba yake anaishi hivyo ndio maana sio injury prone, barafu inasaidia sana japo huku kwetu Mtu anaaza nayo ukubwani, ukimtazama Cristianinho unaweza kuhisi ana bata sana ila anapitia matayarisho makubwa kuvaa viatu vya Baba

Mama yake Georgina ni Mtalaam wa mazoezi pia, familia ina Physio wao pia, si ajabu siku moja baridi na mvua pale Lisbon, ila Ronaldo akaenda na Mwanae uwanjani akimfundisha target na kupiga kwa nguvu, sio ajabu alikuwa anafanya nae mazoezi mazito kipindi cha Karantini

Tazama takwimu zake za Juventus mwaka jana hizo, umegundua niniπŸ˜€

Post a Comment

0 Comments