TUPENDE KUWA KARIBU NA MAADILI YA MUNGU


 

 Huyu ndugu mweusi anaitwa Abel Mutai, ni mwanariadha wa nchi ya Kenya. Wa nyuma yake (huyo mzungu) anaitwa Ivan Fernandez, ni mwanariadha wa Hispania. Mwaka 2013 kwenye mbio za Burlada, Ivan Fernandez alifanya kitendo cha kibinadamu, kimaadili na cha heshima kubwa sana. Hakushinda mbio mahala ambapo kwa tamaa zetu za kibinadamu angeweza kushinda. Ni kwamba, walipokaribia ‘finish line’, Mutai, ambaye alikuwa anaongoza mbio hizo, alikosea sign ya ‘finish line’ akatoka mchezoni kwenye race na kuanza kushangilia kuwa ameshinda, kitendo ambacho kingempa Ivan fursa ya kuwahi kwenye finish line na kuchukua medali ya dhahabu na kumfanya Mutai ajute, alie na kusaga meno. Ivan hakutaka ushindi wa kinyemela, ambao angeupata tu kutokana na makosa ya Mutai. Alimfuata Mutai kule nje na kumrejesha kwenye ‘lane’ huku akimuongelesha kihispaniola kuwa bado hawajafika, japokuwa Mutai alikuwa haelewi lugha hiyo lakini alifuata maelekezo ya Ivan na kufika kituo cha mwisho akachukua ushindi wake. Na Ivan akabaki kwenye nafasi yake ‘halali’ ya ushindi wa pili. Watu hawakumshangilia sana Mutai lakini Walimheshimu sana Ivan. Sababu ikiwa ni moyo wake wa kibinadamu wa kumsukuma Mutai kwenye mstari wa ushindi mpaka akapata haki yake. Ivan alipohojiwa alisema “ndoto yake ni kuona tunajenga jamii ambayo tunasukumana kwenye mstari wa ushindi...”. Mwandishi wa habari akamuuliza, “lakini kwa nini ulimuacha Mkenya akashinda wakati ungeweza kuwa mshindi?”, Ivan alijibu “sikumuachia ushindi. Alikuwa ameshinda. Ushindi ulikuwa haki yake”. Mwandishi akasisitiza, “lakini ungeweza kushinda?”. Ivan akajibu: “lakini ningepata raha gani juu ya ushindi huo? Nini ingekuwa heshima ya medali hiyo? Mama yangu angefikiria nini juu ya hilo?” Mungu atujaaliye tupate watoto wema kama Ivan, watakaokuwa tayari kushinda kwa mbinu halali za ushindi, watakaokuwa tayari kusimama kwenye kanuni za maadili, heshima na uaminifu.

 

Post a Comment

0 Comments