CHAPTER ONE | HUMAN STORIES / CHAPTER ONE| SIMULIZI ZA KIHAMU

 

SIMULIZI NA

CHAPTER ONE | HUMAN STORIES

It was already a very dark night, with terrible rain accompanied by thunder and strong winds so much so that even all the sleep was interrupted

Thick darkness lay in my little room, which my Grandmother had prepared, the battery I had been given had already been turned off by the wind.

I pulled my left hand lazily and clicked on my wristwatch, it was eight-thirty at night, it was very remote and Grandma's house was very isolated.

At that moment my eyes do not see anything, all that is left is the proper use of my ears, despite the sounds of thunder and strong winds I heard a voice coming from inside, the sound was not far from my room

It was like the voice of a middle-aged woman speaking harshly, I heard it from afar, the voice was received by the gentle voice of an old woman.

My body started to get very scared, sweat started to come out of me despite the cold rain, my whole body started to tremble

The first thing I wanted to do was call Grandma but my mouth betrayed me and I became heavy, I wanted to get out of bed, my legs became heavy and betrayed me, my body remained as if I were still dead.

Suddenly it was as if a light was beginning to appear whose direction was the room I was in, a room whose door was just the main main sheet.

The light was coming with two different voices arguing, speaking harshly ......

Don't miss the continuation of this story next Sunday🙏


IN SWAHILI >>


CHAPTER ONE| SIMULIZI ZA KIHAMU

Ni tayari usiku mzito sana, mvua ya kutisha sana ikiambatana na radi na upepo mkali kiasi ambacho hata usingizi wote ulikatika

Giza nene lilitanda kwenye chumba changu kidogo, ambacho niliandaliwa na Bibi yangu, kile kibatari nilichopewa tayari kilizima kutokana na upepo

Nikauvuta mkono wangu wa kushoto kwa uvivu na kubonyeza saa yangu ya mkononi, ilikuwa ni saa nane na robo usiku, ni Kijijini sana na nyumba ya Bibi imejitenga sana

Wakati huo macho yangu hayaoni kitu, kilichosalia ni matumizi sahihi ya masikio yangu, licha ya milio ya radi na upepo mkali nilisikia sauti ikitokea ndani, sauti haikuwa mbali na chumba changu

Ilikuwa kama ni sauti ya Mwanamke wa makamo ikiongea kwa ukali, nilipata kuisikia kwa mbali sana, sauti hiyo ilipokelewa na sauti ya upole ya Mwanamke kikongwe

Mwili wangu ukaanza kujawa na hofu kubwa, jasho zilianza kunitoka licha ya kibaridi cha mvua, mwili mzima ulianza kutetemeka

Kitu cha kwanza nilichotaka kufanya ni kumuita Bibi lakini mdomo ulinisaliti ukawa mzito, nilitaka kutoka kitandani, miguu ikawa mizito ikanisaliti, mwili wangu ulisalia kama Maiti ingali nasikia

Ghafla ni kama kuna mwanga ulikuwa unaanza kujitokeza ambao mwelekeo wake ni chumba nilichopo, chumba ambacho mlango wake ni shuka kuu kuu tu

Mwanga ulikuwa unakuja na sauti mbili tofauti za mabishano, zikisema kwa ukali......

Usikose muendelezo wa simulizi hii Jumapili ijayo🙏

Post a Comment

0 Comments