EVERYTHING IS FINE

 

EVERYTHING IS FINE. 

(Everything is fine.) Kila kitu kipo sawa ila wewe tu ndio haupo sawa kwenye kukitizama kitu hicho. Kila siku milango inafunguka na watu wanapita kutofunguka mlango wako shida si mlango shida ni wewe unaogopa kuufungua mlango wako. Umewahi kufikiri siku ukiamka hauna macho je unafikiri utaishi vipi bila macho?.

Mara zote unaamka asubuhi na kuelekea kwenye shughuli zako utafanyaje siku ukiamka huwezi kuinuka nusu ya mwili wako umepooza. Je utalia?, Utalaumu?, Utatukana? au utaipokea hali uliokuwa nayo na kuanza maisha mapya ya kulala kitandani?. Sihitaji jawabu lako kwasasa nahitaji ufikiri ndio ujijibu wewe mwenyewe.

Je unafahamu kuwa leo sio kama kesho na kesho sio kama jana?. Je unajua kuwa kuna tukio mbele yako ambalo litahitaji ufumbuzi wako?. Everything is fine wewe ndio haupo sawa lakini kila kitu kipo sawa. Kwanini ufikirie kujiua kwa kitu ambacho hata ukiwa nacho bado kitakuwa na changamoto kwako?.

Everything is fine wacha kukatishwa tamaa na watu ambao hawana hata nde kwenye kwenye ustawi wa maisha yako. Leo iwe siku ya kuinuka kwako na kuanza kuishi ndani ya ramani yako na ndoto yako. Mafanikio ni uzao wa changamoto hakuna mafanikio ambayo hayajapitia kwenye changamoto usikate  tamaa Everything is fine don't give up.

#salushine.media

Post a Comment

0 Comments