I have written this to you My Great Son, if you have not read this chana throw it away, and do not tell Natal and Naftary


 

 SIMULIZI 

NA jr_farhanjr

 

 

I have written this to you My Great Son, if you have not read this chana throw it away, and do not tell Natal and Naftary

I am writing to you because you should know why I am going to be buried under the earth due to modern diseases, worldly diseases.

Do you remember the day Naftary hoi was overwhelmed and your mother is my dry tia sauce? I went to cry for Mangi in trouble at the store and mortgaged my body

I remember you asked me Mom why are you crying when we got the money for the Treatment and our Little One is being treated? I wanted to tell you but I smiled at my Son

Remember when you were sent back to College you couldn't do the exam case fees? Your tears were like a knife in my bones, I cried to the Lord David of Hades

What should Mr. David do because his dream was to be with Me, what should I do if I wanted you to read, I mortgaged my body again so you could read

All the time I shed tears before you, and you thought it was tears of joy, but for me it was a joy that you would succeed but sad for me because I will leave My children

Remember the day we didn't have a rent? The landlord's father wants rent? What kind of mother would my children be if you slept outside in the cold? Get bitten by mosquitoes, Small security case of rape?

I followed the landlord, I cried for my problem, what will I give him more than my body? I remember coming back at midnight asleep, my happiness was your safety, though I will leave you with lasting pain

Do you remember My Son at your younger brother's funeral? I couldn’t give away an iPhone gift or a car, we only had two thousand crowns, but what Mother would I be in front of you?

I had to torture my body again, the temple you slept in for nine months, so long as I am the best Mother before you even once, I am thankful I have accomplished that, even though I have stopped the pain in life.

When you put the wreaths on my grave today, then please show him even a smile, then look up at the sky and tell me GOODBYE!

I Love My Sons
Your mother🌹

 

IN SWAHILI

  Nimekuandikia hii wewe Mwanangu Mkubwa, ukishaisoma hii chana utupe mbali, wala usiwaambie Natal na Naftary

Nimekuandikia kwakuwa unapaswa kufahamu kwanini naenda kufukiwa chini ya udongo kutokana na maradhi ya kisasa, maradhi ya kidunia

Unakumbuka ile siku Naftary hoi kazidiwa na Mama yenu ni pangu pa kavu tia mchuzi? Nilienda kumlilia shida Mangi dukani na kuweka mwili wangu rehani

Nakumbuka uliniuliza Mama mbona unalia wakati pesa tumepata ya Matibabu na Mdogo wetu anatibiwa? Nilitamani kukwambia ila nilizuga kwa tabasamu Mwanangu

Unakumbuka umerudishwa Chuo huwezi kufanya mitihani kisa ada? Machozi yako yalikuwa kisu mfupani mwangu, nikampigia Bwana David wa Mashimoni

Afanye nini Bwana David kwakuwa ndoto yake ilikuwa kuwa na Mimi, nifanye nini Mimi ikiwa nilitaka wewe usome, nikaweka tena mwili wangu rehani kisa wewe usome

Muda wote nilitoa machozi mbele yenu, nanyi mkidhani ni machozi ya furaha, bali kwangu ilikuwa furaha kuwa mtafanikiwa ila huzuni kwangu kwakuwa nitawaacha Wanangu

Mnakumbuka ile siku hatuna kodi ya nyumba? Baba Mwenye nyumba anataka kodi? Ningekuwa Mama gani wanangu mkalale nje na baridi kali? Mpigwe na Mbu, usalama Mdogo kisa vibaka?

Nikamfuata Baba mwenye nyumba, nilimlilia shida yangu, nitampa nini zaidi ya mwili wangu? Nakumbuka nilirudi usiku wa manane mkiwa mmelala, furaha yangu ilikuwa usalama wenu, ijapo nitawaachia maumivu ya kudumu

Unakumbuka Mwanangu kwenye mahafari ya Mdogo wako? Sikuweza kutoa zawadi ya iPhone wala gari, tulikuwa na elfu mbili ya mataji pekee, lakini ningekuwa Mama gani mbele yenu?

Nililazimika tena kutesa huu mwili wangu, hekaru mliliolala kwa miezi tisa, ili mradi nami niwe Mama bora mbele yenu hata mara moja, nashukuru nimetimiza hilo, ijapo nimeacha machungu maishani

Mnapoweka Mashada juu ya kaburi langu leo hii, basi naomba muoneshe hata tabasamu, kisha mtazame angani kuniambia GOODBYE!

Nawapenda Wanangu
Mama yenu🌹

 

CLICK HERE TO CONTINUE

Post a Comment

0 Comments